Elimu ya Biashara na Uchumi

Elimu ya Biashara na Uchumi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Elimu ya Biashara na Uchumi, Kyela.

29/10/2024
Tuambie unafanya biashara gani, inayokulipa ili umshawishi na mwenzako ambae Hana biashara yoyote apate plani????
21/03/2023

Tuambie unafanya biashara gani, inayokulipa ili umshawishi na mwenzako ambae Hana biashara yoyote apate plani????

ZIFAHAMU AINA TANO ZA UWEKEZAJI© 2020 AMKA MTANZANIA   Ili kuweza kuwa na utajiri endelevu katika maisha yako na unaoj...
01/08/2020

ZIFAHAMU AINA TANO ZA UWEKEZAJI

© 2020 AMKA MTANZANIA   Ili kuweza kuwa na utajiri endelevu katika maisha yako na unaojitosheleza ni muhimu ukawa mwekezaji. Uwekezaji upo wa aina nyingi. Hapa ninakuletea aina za uwekezaji unazoweza ku*ifanya ili kukuwezesha wewe na wale watu wako wa karibu kuishi maisha ya utajiri wa kujitosheleza:
1. Uwekezaji binafsi
Watu ambao wanatengeza utajiri wanafanya uwekezaji binafsi . hawa wanakuwa wasomaji kwa kujifunza. Daima huweka jitihada ya kujiboresha wao wenyewe siku hadi siku na kuongeza mipaka ya maeneo ambayo wanona wakijaribu watafanikiwa. Wanaongeza maarifa na uwezo wa kushawishi siku hadi siku. Na kiwango cha jitihada wanachoweka katika kujiboresha huwa kipo katika hali ya kukua siku hadi siku.
2. Kuwekeza kwa wengine
Mwanamafanikio maarufu duniani Zig Ziglar alisema ukitaka kupata kitu chochote katika maisha ni vizuri uwasaidie wengine wapate vile wanavyovihitaji katika maisha yao. Watu wenye utajiri utagundua wamewekeza kuwasaidia wengine wafikie malengo yao na hivyo kusababisha na wao kufanikiwa kwa kuwa
3. Wekeza katika taasisi
Katika taasisi unayofanya wekeza katika kuijenga taasisi hiyo ili iweze kuwa bora na taasisi inapoweza kuwa bora inawezesha kuongeza upataji wa mapato. Kuongezeka kwa mapato kwa taasisi kwa ujumla kunasaidia pia wale waliosababisha kuongezeka kwa mapato kuneemeka na hiyo faida. Kwa hivyo hili likifanyika katika kipindi chako cha kutumikia taasisi yako maanake utaongeza kujenga utajiri siku hadi siku.
4. Wekeza katika mali zinazoongezeka thamani
Ubadilishaji wa fedha kwenda katika mali ambazo zinaongezeka thamani na zinafanya kazi badala yako siku hadi siku huongeza utajiri kwako. Mfano wa hili ni nyumba ambayo imejengwa kwa lengo la kupangasha au kukodisha. Sasa ile fedha uliyowekeza katika hiyo nyumba utaipata kwa kuendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka bila yaw ewe kufanya kazi.
5. Wekeza katika mawazo
Vitu vingi tunavyoviona leo havikuanza moja kwa moja bila kupitia hatua Fulani, vingi vilianza k**a wazo na kuendelezwa. Mawazo amabyo ni mazuri yakichanganywa na uchukuaji hatua wa kuyaweka katika matendo huleta matokeo mazuri ambayo yanaleta utajiri

NJIA 10 ZA KUWEKA AKIBA (SAVING OPTIONS) ZENYE KUFUATA MASHARTI YA KIISLAM (Sharia compliant).By Salum Awadh, SSC Capita...
02/07/2020

NJIA 10 ZA KUWEKA AKIBA (SAVING OPTIONS) ZENYE KUFUATA MASHARTI YA KIISLAM (Sharia compliant).

By Salum Awadh, SSC Capital.

Ni vugumu kufanikiwa kifedha (financial success) na kuwa huru kifedha (financial freedom), k**a hatuwezi;
- Kukuza vipato
- Kuweka akiba
- Kuwekeza akiba zetu

Njia zipo nyingi, ila ni muhimu kujua ni njia zipi zinakubalika kisharia, na hii ni muhimu kwa wote mjasiriamali na mwajiriwa;.

1. Kuweka akiba ya muda mrefu
- Hii ni muhimu k**a una malengo ya muda fulani ujao na huna hakika k**a utakuwa na fedha katika kipindi hicho. Utafanya hivyo kwa kufungua akaunti ya benki kwa kipindi maalum (fixed deposit) yenye tija pia ya kupata gawio la faida. Tembelea benki za kiislam k**a Amana, KCB, NBC, na PBZ kwa maelezo zaidi.

2. Kuwa na bima

Sheria ya kiislam imeweka utaratibu wa bima ya kiislam k**a kinga ya majanga ambayo yanaweza kutokea na wewe kushindwa kuyamudu kwa kukosa akiba muda huo. Utaratibu wa bima ya kiislam unaitwa Takaful, na utaanza muda c mrefu nchini Tanzania, fuatilia taarifa hizi kwa karibu ili uweze kujiunga

3. Wekeza akiba yako

Zipi njia nyingi zinazokubalika kisharia kuwekeza akiba yako bila wewe kufanya kazi ya uzalishaji wa faida ya shughuli husika (Passive investments). Njia hizi ni pamoja na kununua hisa (shares), kuwekeza kwenye masoko ya mitaji ya mikopo (bonds), au kuwekeza kwa njia ya mifumo ya kununua vipande (unit trusts). Uislam pia umeweka utaratibu wa aina za hisa za kununua (sharia complaint shares/stocks), Sukuk (islamic bonds), na sharia compliant mutual funds. Hizi kwa Tanzania hamna kwa sasa, ila unaweza kununua kwenye nchi nyingine k**a Malaysia, Dubai, Bahrain, UAE, n.k, unaweza kutumia kampuni ya Wahed kwa ku download app yao na kujisajili

4. Kununua bidhaa za thamani k**a vile dhahabu na silver, na ku*iweka. Na bdae ku*iuza unapohitaji fedha kwa mahitaji yako. Omba ushauri zaidi kwa wataalam wa sharia kwenye hili.
5. Kufungua akaunti za malengo. Huu ni utaratibu wa mabenki ambao unakusaidia kufungua akaunti maalum kwa malengo maalum k**a vile malengo ya kwenda hajj, akaunti za watoto kuandaa ada za shule, n.k

6. Kujiunga na mifuko ya kijamii (social security schemes). Hii inakusaidia kuwa na akiba ya kukuwezesha kukidhi mahitaji kipindi ambacho huwezi kuwa na chanzo kingine cha mapato, k**a vile ukistaafu, ukipata ulemavu wa kudumu, au kufikwa na mauti na wategemezi wako kuendelea kupata mahitaji yao. Upo utaratibu wa kisharia juu ya mifumo hii, ongea na wataalum wa sharia kukushauri zaidi kabla ya kujiunga.

7. Kutengeneza mfuko wa familia wa waqf ( Family trust)/ ( Al-waqf al-’ahli).
Kwa utaratibu huu unaweza kusajili waqf na kuweka kiasi cha fedha ambacho kinaweza kuwanufaisha wategemezi wako. Mfuko huu unakuwa unasimamiwa na mtaalam (Trustee/mutawalli), ambaye atawajibika kuutunza, kuukuza, na kukidhi mahitaji ya wategemezi yatakoidhinishwa na mtoaji (Waqif)
8. Kuwekeza kwenye mifumo ya umiliki wa pamoja wa majengo (Real estate investment trusts (REITs).
Huu ni utaratibu ambao unanunua hisa kwenye kampuni ya real estate iliyoanzishwa maalum kwa ajili ya kuwekeza kwenye majengo (real estate), kampuni inasimamiwa na mtaalam, na kila mwisho wa mwaka faida inayotokana na kipato cha kodi, kinagawiwa wanahisa k**a gawio (dividend), unaweza kufanya hivi pia kwa kuwekeza kwa njia ya crowdfunding inayojihusisha na miradi ya ujenzi tu k**a vile ethiscrowd.com iliyopo singapore, inayozingatia sheria ya kiislam.
9. Kujiunga na utaratibu wa vyama vya kuweka na kukopa (saccos) au benki za kijamii (Village community banks(VICOBA). Hii ni nzuri zaidi kwenye vipato vidogo. Hakikisha kabla hujajiunga kuwa chama hicho kinaendeshwa kwa misingi ya kiislam ikiwemo kutotoza riba katika miamala yake.
10. Usiweke fedha kwenye kibubu. Watu wengi wamekuwa na tabia ya kuweka fedha kwenye kibubu, hii si njia salama na si njia bora kuweka akiba. Hali hatarishi (risks) zipo nyingi k**a vile kuibiwa, kushika moto, kuingia maji, kupata tamaa ya kukivunja, na pesa kutoweza kuwekwa kwenye njia mbadala ambazo utaweza kuweka akiba na utapata faida.

HITIMISHO

Ili uweze kufanikiwa katika haya, hakikisha;
1: unasoma majarida ya mifumo ya fedha na uwekezaji wa kiislam mara kwa mara
2. Omba ushauri kwa wataalum wa fedha na uwekezaji
3. Omba ushauri kwa wataalum wa sharia ( sharia scholars)
4. Hudhuria mafunzo na makongamano
5. Jifunze elimu ya bajeti, vipato, na matumizi
6. Jitahidi kuishi chini ya kipato chako ili uweze kubaki na akiba
7. Jua tofauti ya majitaji na matakwa ( needs and wants)
8. Fahamu kuwa akiba yako na kipato chako kitalizimika kutolewa zaka, pale ambapo zikikidhi masharti na viwango. Pata ushauri kwa wataaalm wa sharia

UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MICHEA)MAHITAJI:- Kostik soda ya unga au ya mabonge                          Maji safi        ...
18/04/2020

UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MICHE
A)MAHITAJI:- Kostik soda ya unga au ya mabonge
Maji safi
Mafuta ya mise/pamba/nazi/mawese n.k
Rangi ya kutengenezea sabuni za miche(blue/pink/kijani n.k
Marashi upendayo lemon/apple n.k
Tanbihi:k**a unata kutengeneza sabuni za tiba(virutubisho)utahitaji kuwa na kirutubisho unacho taka kutumia kwa mf:Aloe Vera/Ubuyu/Papai/Mwarobaini n.k
Box la kutengenezea sabuni na vibao vya kukatia sabuni vyenye ukubwa wa mche wa sabuni.
Ndoo kubwa za maji angalau 3 na ndoo ndogo 3,conduse ya plastiki kwa ajili ya kukorogea.Sodium Siliket,magadi soda,Hydrometa nzito pamoja na meza ya kukatia sabuni.

Kanuni:-kostik kg 1
Maji lita 3
Mafuta lita 6
Sodium siliket grm 500
Magadi soda vijiko vikubwa vya chakula 10
Rangi kijiko 1 cha chakula
Pia utahitaji eneo la kufanyia kazi pamoja na rasilimali watu angalau wawili.
Loweka kostik soda kwa masaa 24,kasha ikoroge na uipime nguvu yake kwa kutumia hydrometa iwe bomee 25-30bm
Ikiwa imezidi bm 30 haifai kwa matumizi ya binadamu ipunguze nguvu kwa kuongeza maji kiasi na upime tena,chukua ndoo ndogo ya maji na uweke mafuta,soda ash,sodium siliket,manukato na uchukue mafuta kidogo uweke kwenye spray(kiasi cha nusu lita)na uchananye na rangi au virutubisho na ukoroge vizuri baada ya kukoroga vizuri changanya na kostik soda koroga tena mpaka ichanganyike vizuri weka nailoni laini kwenye box kuzuia mchanganyo wa sabuni kumwagika(kuvuja) anza kupulizia rangi kwenye box na endelea kumimina mkorogo(mchanganyo wa sabuni kidogo kidogo huku ukiendelea kupulizia rangi kwa awamu mpaka mwisho mwisho weka contena la sabuni(box)kwenye sehemu nzuri ambapo ardhi imenyooka na usubiri kwa masaa 24 bonge la sabuni litakuwa tayari kukatwa na ili sabuni ikauke vizuro anika chini kwenye sakafu lakini tanguliza magazeti na chumba kisiwe chenye kuingiza mwanga wa jua.

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI1. Chukua sulphonic 1 lita moja weka katika chombo chako cha kutengenezea(lita 25) .2...
02/04/2020

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI
1. Chukua sulphonic 1 lita moja weka katika chombo chako cha kutengenezea(lita 25) .
2. Kisha chukua slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka sulphonic kisha changanya kwa pamoja.
3. Chukua soda ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine pembeni , kisha chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako chenye mchanganyiko wasulphonic na sles weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10 kuwa makini kwasababu utavimba sana.
4. Kisha weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi kutokana na rangi unayoitaka lakini angalia isizidi sana koroga tena vizuri.
5. Kisha chukua glycerin vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana.
6. Kisha weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) , hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri.
7. Koroga chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu k**a vijiko 6 ya chai kisha mimina katika mchanganyiko wako naKisha weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) , hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri
NB , Chumvi ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwahiyo kuwa makini sana.
8. Kisha weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuweka formalin kisha koroga tena vizuri. (alka na formalin sio lazima sana hata k**a hautavitumia sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).
ANGALIZO
1. Mchanganyiko wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa makini.
2. Kuna baadhi ya malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga k**a Maski na Gloves.

22/03/2020

HII NDIO NAMNA YA KUJUA JINSI BIASHARA YAKO INAVYOWEZA KURUDISHA PESA ZAKO ULIZO TUMIA,

Kwa kawaida kila mtu anapowekeza pesa zake hutegemea kupata faida au kwa lugha nyingine unaweza ukasema anataka biashara au mradi umlipe. Biashara isiyolipa maarufu k**a “Biashara kichaa” hamna mtu atataka kuifanya hata kidogo. Faida au kulipa kwa biashara ndiyo “uchawi” wenyewe nyuma ya uwekezaji wowote ule duniani kote. Katika Ulimwengu wa biashara kuna kitu kinachoitwa Return On Investment(ROI), tafsiri yake isiyo rasmi unaweza kuita, Malipo katika Uwekezaji, kuna wanaoita pia Rate Of Return(ROR). ROI au ROR maneno hayo ya kitaalamu yasikutishe, siyo kitu cha ajabu sana bali tu ni KIWANGO CHA ULIPAJI wa biashara husika ambacho ni uwiano unaopimwa katika asilimia kuonyesha kiwango chake cha ufanisi (business performance) Unataka kujua ni kwa asilimia ngapi fedha utakazowekeza zinaweza kutengeneza faida katika kipindi fulani tuseme labda mwaka nk. SOMA: Ijue sehemu ngumu kuliko zote unapoandika mchanganuo wa biashara yako. ROI kanuni yake ni hii, Unachukua Thamani ya mradi baada ya kupata faida Unatoa Gharama zote za mradi, jibu gawa kwa Gharama za mradi kisha u*idishe mara 100. Tuchukulie mfano umeanzisha biashara ya kutengeneza juisi ya ubuyu, Gharama zote za kuanza ni sh. 20,000 Baada ya kuuza juisi yote faida ukapata ni sh. 4,000 Hivyo ROI yako itakuwa (4,000/20,000) X 100 = 20% Ukiweka pesa kwenye akaunti, fixed deposit sh. Milioni 10 baada ya mwaka ukakuta imeongezeka sh. Laki 5 ina maana kwamba ROI yako ni (500,000/10,000,000)x100 = 5% Hivyo biashara hii ya juisi ya ukwaju kiwango chake cha ulipaji ni kizuri tu asilimia 20% ingawa hatujazingatia muda k**a mwaka mmoja nk. Kuna biashara huwa na kiwango cha chini sana kwa mfano ukiwekeza pesa zako katika akaunti za kudumu katika mabenki huwezi ukapata zaidi ya asilimia 5% kwa mwaka, hisa katika makampuni ni wastani wa asilimia 10%, Majengo wastani asilimia 10% nk. SOMA: Makisio ya fedha kwenye mpango wa biashara. Asilimia kubwa maana yake biashara inalipa sana na asilimia ndogo biashara inalipa kidogo. Tukiwa tunaelekea siku ya semina yetu kubwa ya HESABU ZA MCHANGANUO WA BIASHARA Machi 29mwaka huu, leo nimeanza kukuletea vidokezo na dondoo mbalimbali k**a matayarisho ya semina hiyo. Kipimo hiki ROI ni muhimu sana kwani unaweza ukalinganisha biashara tofauti unazofikiria kuanzisha ukachagua moja iliyo na kiwango(ROI) kikubwa zaidi. Uwiano wa ROI pamoja na vipimo vingine vingi tutakwenda kujifunza vyote kwa kina katika semina hiyo kwa lugha rahisi kabisa mtu wa kawaida anayoweza kuelewa. Uwiano huu unakuwezesha kujua biashara inalipa vizuri kwa kiasi gani(Business Performance) Hata hivyo katika kuchagua biashara ya mtu atakayoifanya kuna vigezo vingine mbalimbali ndio maana unaweza kukuta biashara ina ROI kubwa tu lakini bado watu wanashindwa au wanaogopa ku*ifanya na wanapoamua ku*ifanya bila ku*ingatia vigezo hivyo vingine huishia kupata matokeo mabaya ambayo hawakuyatarajia.

NB.
(Kupata iyo elimu ingekubidi ulipe kiasi si chini ya million moja vyuoni)

15/03/2020

INTRODUCTION TO ECONOMICS

jifunze uchumi kwa ufupi..

UCHUMI, ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Ni hasa
uzalishaji , usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.

Uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za
kijiji , eneo , taifa au dunia .
Sayansi ya Uchumi (kwa Kiingereza economics) ni tawi la elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.

Sekta za uchumi
Uchumi wa jadi katika nchi nyingi ulikuwa hasa
kilimo cha kujikimu pamoja na biashara ya kubadilishana bidhaa kadhaa zenye thamani kubwa. Kwa mfano, tangu kale migodi ya
Zimbabwe ilichimba dhahabu iliyopelekwa baadaye hadi Asia na kando ya Mediteranea .
Katika uchumi wa kisasa mara nyingi sekta tatu hutofautishwa:

Sekta ya msingi: kutoa na kuzaa malighafi pamoja na mazao katika mazingira asilia. Mifano ni kilimo, uchimbaji wa madini , uvuvi au kuvuna ubao .

Sekta ya pili: shughuli za kubadilisha malighafi hizi kuwa bidhaa. Madini ya chuma hubadilishwa kuwa feleji ; feleji hutumiwa na
viwanda kutengeneza vyuma vya ujenzi ,
magari , vifaa vya nyumbani . Viwanda vya
nguo hutumia pamba kutoka mashambani na kuibadilisha kuwa u*i halafu kitambaa na nguo.

Sekta ya tatu: biashara au usambazaji wa bidhaa hizi kwa wateja pamoja na kuwatolea huduma. Mifano ni maduka yanayouza bidhaa zilizotengenezwa viwandani. Mingine ni huduma k**a benki, hoteli, sinema na
usafiri.

Wataalamu wengine hutaja sekta ya nne: shughuli za kusambaza habari na pia utafiti wa teknolojia mpya unaoendelea kuwa muhimu katika nchi zinazoendelea . Wengine huingiza pia elimu (kazi za shule na vyuo ) katika sekta hii ya uchumi.

TUKUTANE DARASA LIJALO......TAFADHADRI FOLLOW PAGE YETU

Address

Kyela

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elimu ya Biashara na Uchumi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share